Mke WA Frank anajivunia mume mtulivu, hashindi baa na hatongozi
videmu. Akitoka kazini huenda kucheza basketball na hurudi nyakati za
dinner. Siku moja mkewe akamhurumia. Anachoka na kazi. Mtu gani
asiyependa starehe japo kidogo? Mke akamlazimisha outing, Frank
akabisha lakini taxi ikafika. Gonga Club & Lodge.
Walipofika mlangoni tu, mlinzi akaita, “Mambo Frank!” “Poa”
“Nilidhani huwa huji club, inakuwaje mlinzi anakufahamu?” mke akauliza
“Yule mgambo, mchana analinda ofisini kwetu, usiku anapiga part time
hapa” akajibu Frank
Wakachagua meza. Kukaa tu tayari mhudumu ameshaleta castle lager.
Akamuuliza mama anakunywa nini. Mhudumu alipoondoka mama akauliza,
“amejuaje unakunywa castle kama hakufahamu?”
Wakati Frank anajikanyaga aanze vipi kujitetea, mhudumu wa vyumba
akawa amefika na kuuliza.
“Mkuu kama kawaida nimekuandalia namba tano, nendeni tu vinywaji
nitawaletea huko huko”
Kufikia hapo mama akawa hana simile tena, akanyanyuka akitukana kama
chizi. Akatoka nje mbio na kuingia katika taxi iliyokuwepo pale.
Wakati anapatana bei na dereva, Frank naye akaingia. Mama
yakamporomoka matusi kibao na kilio juu. Alipovuta kamasi na kupiga
kwikwi akamsikia dereve anasema.
“Duh, eee bwana Frank huyu wa leo uliyemuokota leo balaaaaaaaaaaaaaaa!”
mamaa akazimiaaaazzzzzzzzzzzzzzzzzzzz
0 comments:
Post a Comment